Mkuki Na Nyota Publishers

Machozi Yamenishiya

Author(s): diwani, fasihi ya Kiafrika, Kiswahili, Mabati-Cornell, Mohammed Ghassani, siasa, ushairi, Zanzibar

Sh 15,000

Diwani ya mashairi ya Kiswahili ya Mohammed Khelef Ghassani, mshairi kutoka Zanzibar aliyeshinda Tuzo ya Fasihi ya Kiafrika kwa Lugha ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya 2015 kwa diwani yake N’na Kwetu. Mashairi yanayoangazia mateso, maumivu, na siasa kwa weledi wa kisanaa.

Diwani ya mashairi ya Kiswahili ya Mohammed Khelef Ghassani. Mateso, maumivu, na siasa ni mambo yaliyojaa uchochezi mkali unaomsukuma mshairi kuzungumza waziwazi na kinagaubaga, na hatimaye kumfanya mwandishi apandwe na jazba zinazofanya kazi fulani itoke nje ya kingo za ulingo wa kisanaa. Mshairi lazima atunge wimbo unaoimbika ndani ya nafsi yake mwenyewe kwanza, wimbo utakaomwezesha kunyanyuka kitandani asubuhi huku akijua hayuko pweke, ana wenzake wenye maumivu kama au kuliko yake. Mohammed Ghassani ana weledi huu wa kubaki ndani ya kingo za ulingo wa kisanaa, weledi wa kuichenga siasa kwa namna ya kuipa nguvu kubwa zinazoficha na kuzimua unagaubaga na ukali wake. Mwandishi alizaliwa mwaka 1977 visiwani Zanzibar na ametunga diwani kadhaa; diwani yake N’na Kwetu ilimpatia Tuzo ya Fasihi ya Kiafrika kwa Lugha ya Kiswahili ya Mabati-Cornell mwaka 2015.

Weight 0.5 kg
Dimensions 230 × 150 mm
Binding

Pages

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Machozi Yamenishiya”

Your email address will not be published. Required fields are marked *