Diwani ya ushairi ya Kiswahili iliyoandikwa na Ally Bakari Mchanyato, mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Kiswahili ya Safal-Cornell ya Fasihi ya Afrika ya mwaka 2023 katika kipengele cha ushairi. Mbali na dhana iliyotawala kwenye jamii kwamba Uswahilini ni sehemu iliyosheheni vituko na maovu yaliyokubuhu, na misemo iliyoenea kuwa Waswahili ni watu wasioishiwa visa na mikasa, mwandishi wa diwani hii ameukumbatia Uswahili kwa kuimulika hali halisi ya maisha yaliyopo na mambo yatokeayo: mapenzi, elimu na mbinu za kuitafuta, siasa, dini na nasaha zake njema, mbinu za kujikwamua kiuchumi, malezi, na haki za wanawake. Waswahili si watu wa kubezwa na kushushwa hadhi. Hakika Uswahilini kuna mengi mazuri ya kuwasaidia Waswahili na jamii zinazochangamana nao. Mchanyato ni mzaliwa wa Ilala jijini Dar es Salaam, mjasiriamali aliyeanza kuandika mwaka 1998.

Uswahilini
Author(s): Ally Bakari Mchanyato, Dar es Salaam, diwani, Ilala, Kiswahili, Safal-Cornell 2023, ushairi, Uswahilini
Sh 18,000
Diwani ya ushairi ya Kiswahili ya Ally Bakari Mchanyato, mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Safal-Cornell 2023 katika kipengele cha ushairi. Inampinga dhana ya uswahilini kama sehemu ya vituko na inamulika hali halisi: mapenzi, elimu, siasa, dini, uchumi, malezi, na haki za wanawake. Mwandishi kutoka Ilala.
| Dimensions | 195 × 130 mm |
|---|---|
| Binding |
You may also like…
-

The African Epic Controversy
Sh 45,000




Reviews
There are no reviews yet.