Mkuki Na Nyota Publishers

Mfinyanzi Aingia Kasri

Author(s): Kiswahili, muziki, Nasra Mohamed Hilal, Siti Binti Saad, Taarab, Unguja, wasifu, Zanzibar

Sh 8,000

Wasifu wa Kiswahili wa Siti Binti Saad, Malkia wa Taarab, iliyoandikwa na Nasra Mohamed Hilal. Mwimbaji kutoka Unguja aliyeupa muziki wa Taarab sura mpya na kuufikisha katika ngazi ya kimataifa. Earlier biography Wasifu wa Siti Binti Saad was written by Shaaban Robert. Internationally distributed by African Books Collective.

Wasifu wa Siti Binti Saad, mzaliwa wa Unguja, aliyejulikana kama Malkia wa Taarab. Umeandikwa na Nasra Mohamed Hilal. Wapenzi wa muziki wa Taarab wana deni kubwa kwa mwimbaji huyu maarufu ambaye, katika uhai wake na baadaye, aliuchukua muziki wa Taarab, akaupa sura mpya, akaubeba, na kuufikisha katika ngazi ya kimataifa. Licha ya kuwa waimbaji wengi wa Taarab wamekuja na kuondoka, hakuna ambaye amefikia kilele alichofika Siti Binti Saad. Hayati Shaaban Robert, ambaye naye alikuwa na kipaji cha pekee katika uwanja wa ushairi wa Kiswahili, alihusudu uimbaji wake na kushangilia maendeleo yake kiasi cha kuandika kitabu juu yake kiitwacho Wasifu wa Siti Binti Saad. Kitabu cha Nasra Mohamed Hilal ni wasifu wa kisasa wa Malkia huyu maarufu wa Taarab.

Dimensions 207 × 145 mm
Binding

Pages

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Mfinyanzi Aingia Kasri”

Your email address will not be published. Required fields are marked *