Mkuki Na Nyota Publishers

Mungu Hakopeshwi

Author(s): Kiswahili, Mabati-Cornell, riwaya, Safal-Cornell, tuzo ya fasihi, Unguja, Zainab Alwi Baharoon, Zanzibar

Sh 20,000

Riwaya ya kwanza ya Zainab Alwi Baharoon kutoka Mji Mkongwe Zanzibar, iliyoshinda Tuzo ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika ya 2018. Inafuatilia familia ya Unguja iliyoingia mitafaruku kutokana na siri za baba, Bw. Ahmed. Lugha fasaha ya Kiunguja na uchambuzi wa mapambano ya wanawake dhidi ya ubabaitani wa Kiume.

Riwaya ya Kiswahili iliyoandikwa na Zainab Alwi Baharoon, mzaliwa wa Mji Mkongwe Zanzibar. Riwaya hii ilishinda na kupewa Tuzo ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika kwa mwaka 2018. Inaelezea maisha ya familia moja ya Unguja iliyoingia katika mitafaruku na mikasa mingi. Kila kitu huwa na chanzo na khatima, na hadithi inachunguza chanzo cha mitafaruku hiyo na khatima yake. Simulizi ni juu ya baba, Bw. Ahmed, mwenye hasira kali zisizo na mipaka, aliyeongoza familia yake kwa utashi wa nafsi yake, bila kujali hisia za mkewe wala wanawe. Moyoni mwake alihifadhi siri, na hiyo siri ndiyo iliyomfanya kuwa mkali bila kiasi, ikimsukuma azuie kurejea kwa yale yaliyomfika zamani. Lakini kivuli cha historia ya maisha yake ya nyuma hakikuacha kumuandama. Riwaya imeandikwa kwa lugha nzuri na fasaha ya Kiunguja, kwa ufundi wa msanii makini na mwelewa wa jamii za Kizanzibari.

Weight 0.5 kg
Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Pages

Year published

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Mungu Hakopeshwi”

Your email address will not be published. Required fields are marked *