Mkuki Na Nyota Publishers

Mmeza Fupa

Author(s): Ali Hilal Ali, Kiswahili, Mabati-Cornell, Pemba, riwaya, Safal-Cornell, tuzo ya fasihi, Zanzibar

Sh 18,000

Riwaya ya Kiswahili ya Ali Hilal Ali kutoka Pemba, Zanzibar, iliyoshinda Tuzo ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika ya 2017. Bi. Msiri anaponea chupuchupu kuteketezwa na familia yake, na baadaye anasimulia mengi yaliyotiwa kapuni. Lugha fasaha na wahusika waliobuniwa kwa ustadi, wenye mikinzano ya kihistoria na kitamaduni.

Riwaya ya Kiswahili iliyoandikwa na Ali Hilal Ali, mzaliwa wa Kisiwani Pemba, Zanzibar. Riwaya hii ilishinda na kupewa Tuzo ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika kwa mwaka 2017. Katika tangazo la ushindi, jopo la majaji lilielezea kwamba si mno mtu kukutana na riwaya ya Kiswahili ambayo mwandishi wake amejidhihirisha kuwa ni mbuji wa lugha fasaha na ya kisanii, inayotiririka kitabia kwa hiari yake, bila dalili zozote kwamba imelazimishwa. Wahusika wote wamebuniwa kwa ustadi, na kupewa kazi mwafaka za kuziwakilisha tanzu na matabaka mbalimbali ya jamii, pamoja na mikinzano yao ya kihistoria, kisiasa, kisaikolojia, na kitamaduni. Ingawa matukio yanatokea katika kisiwa cha kubuni, masuala yanayojadiliwa ni miongoni mwa yale sugu yanayoendelea kulisumbua bara la Afrika kisiasa, kijamii, na kiuchumi. Riwaya inafuatilia Bi. Msiri, aliyeponea chupuchupu kuteketezwa pamoja na familia yake, na jinsi anavyokuja kuyasimulia mengi yaliyotiwa kapuni.

Weight 0.5 kg
Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Pages

Year published

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Mmeza Fupa”

Your email address will not be published. Required fields are marked *