Mkuki Na Nyota Publishers

Mapenzi Bora

Author(s): classic, diwani, fasihi ya Kiswahili, Kiswahili, mapenzi, mshairi wa taifa, Shaaban Robert, ushairi

Sh 7,000

Diwani ya mashairi ya Shaaban Robert, mshairi wa taifa wa Kiswahili, yenye kichwa Mapenzi Bora (Worthy Love). Sehemu ya jitihada ya kuvichapisha tena vitabu vya mwandishi huyu aliyelinganishwa na Shakespeare kwa lugha ya Kiingereza, baada ya zaidi ya miaka kumi na tano kukosekana Tanzania. Internationally distributed by African Books Collective.

Diwani ya mashairi ya Sheikh Shaaban Robert yenye kichwa Mapenzi Bora (Worthy Love). Shaaban Robert ni mwandishi maarufu kushinda wote katika jamii za Waswahili kote Afrika ya Mashariki na Kati. Kwa zaidi ya miaka kumi na tano, vitabu vyake havikupatikana Tanzania kwa sababu kampuni ya kigeni iliyovichapisha iliacha kuvichapisha kutokana na hali mbaya ya uchumi. Athari ya kupotea kwa vitabu vyake ni kwamba Watanzania wengi, hasa wenye umri chini ya miaka thelathini, hawamjui mwandishi huyu maarufu na hawakulelewa katika mazingira ya utajiri wa maandishi yake. Kwa kuvichapisha tena vitabu vya Marehemu Sheikh Shaaban Robert, Watanzania, hasa vijana, wanakaribishwa tena kuvisoma. Shaaban Robert kwa lugha ya Kiswahili ni sawa na Shakespeare kwa lugha ya Kiingereza, mshairi wa taifa ambaye vitabu vyake daima vimekuwa kipimo cha juu cha uhondo wa lugha, usafi wa nia, na hekima.

Weight 0.2 kg
Dimensions 208 × 147 mm
Binding

Pages

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Mapenzi Bora”

Your email address will not be published. Required fields are marked *