Diwani ya ushairi ya Kiswahili iliyoandikwa na Mohammed K. Ghassani, mshindi wa Tuzo ya Safal-Cornell. Tungo nyingi zilizomo humu ziliandikwa baina ya robo ya mwisho ya mwaka 2010 na nusu ya mwanzo ya mwaka 2015; miaka mitano ya kwanza ya mshairi kuhamia na kuishi nchini Ujerumani, mbali na nyumbani kwao Zanzibar. Ndani yake muna muakisiko wa hisia za mgeni ugenini, akitayamani mengi mazuri ya kwao na akijutia kuyaacha nyuma yake. Ukweli ni kuwa wakati mtu anapoishi ugenini, ndipo hasa ile thamani ya kwao anapoitambua na kutaka kujitambulisha nayo zaidi na zaidi. Kutoka kipembe cha mbali, Ghassani anakiangalia kwao na kuyaona mambo ambayo alipokuwamo ndani yake, alikuwa hata hajui kama yapo. Chembilecho Wajapani, samaki hajijui kuwa amerowa, kwani yeye mwenyewe anaishi ndani ya maji muda wote. Ghassani alizaliwa kisiwani mwaka 1977, alihamia Unguja 1996, na Ujerumani 2010.

N’na Kwetu
Author(s): diwani, Kiswahili, Mohammed K. Ghassani, Safal-Cornell, ugenini, Ujerumani, ushairi, Zanzibar
Sh 15,000
Diwani ya ushairi ya Kiswahili ya Mohammed K. Ghassani, mshindi wa Tuzo ya Safal-Cornell. Tungo zilizoandikwa kati ya 2010 na 2015, miaka ya kwanza ya mshairi nchini Ujerumani. Ushairi wa nyumbani kutoka kipembe cha mbali; mgeni anayeelewa thamani ya kwao zaidi akiwa ugenini.
ISBN: 9789987537703
Category: Poetry
Tags: diwani, Kiswahili, Mohammed K. Ghassani, Safal-Cornell, ugenini, Ujerumani, ushairi, Zanzibar
| Dimensions | 195 × 130 mm |
|---|---|
| Binding |
Be the first to review “N’na Kwetu”Cancel Reply
You may also like…
Related products
-

Bure Ghali
Sh 10,000 -

Mzoga Unaonukia
Sh 12,000 -

Mmeza Fupa
Sh 18,000 -

Moto wa Kifuu
Sh 10,000

Reviews
There are no reviews yet.