Diwani ya mashairi ya Kiswahili iliyoandikwa na Dotto Rangimoto. Imetunukiwa Tuzo ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika kwa lugha ya Kiswahili. Majaji walioisoma ni Ken Walibora Waliaula (Mwenyekiti), Daulat Abdalla Said (Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar), na Ali Attas (Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Japan). Mashairi yaliyomo yametumia lugha iliyojaa taswira na majazanda yanayowakilisha vyema hisia zinazoelezwa katika dhamira mbalimbali. Mshairi amefaulu sana kuzitumia mbinu na miundo mbalimbali kuyajadili maswala yanayohusu hali na mazingira tofauti tofauti katika maisha ya binadamu. Anayazungumza maswala mazito lakini kwa namna ambayo hayamuelemei msomaji wake, badala yake humshawishi aendelee kuyasoma. Hata yale maswala makongwe, kwa mfano uhusiano baina ya wazazi na wana wao, yanajadiliwa kwa namna ya kuvutia. Dotto Rangimoto ni mtunzi stadi, na diwani hii ni mchango mkubwa katika ushairi wa Kiswahili wa zama zetu.

Mwanangu Rudi Nyumbani
Author(s): diwani, Dotto Rangimoto, Kiswahili, Mabati-Cornell, mashairi ya kisasa, Safal-Cornell, tuzo ya fasihi, ushairi
Sh 10,000
Diwani ya mashairi ya Kiswahili ya Dotto Rangimoto, iliyoshinda Tuzo ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika. Mashairi yaliyojaa taswira na majazanda, yanayojadili hali za maisha ya binadamu kwa njia inayovutia. Uhusiano wa wazazi na wana, pamoja na maswala mazito ya kisasa, yamewasilishwa kwa lugha fasaha.




Reviews
There are no reviews yet.