Mkuki Na Nyota Publishers

Mji Wa kambare

Author(s): diwani, Kiswahili, lahaja ya kipemba, lugha ya picha, Rashid Othman Ali, Safal-Cornell, ushairi, Zanzibar

Sh 15,000

Diwani ya ushairi ya Kiswahili ya Rashid Othman Ali, mshindi wa Tuzo ya Safal-Cornell, iliyoandikwa kwa lahaja ya kipemba. Inalenga wapenzi wa mashairi, wanaisimu, walimu, wakufunzi, na vikundi vya sanaa. Maneno magumu yamefafanuliwa mwishoni.

Diwani ya ushairi ya Kiswahili iliyoandikwa na Rashid Othman Ali, mshindi wa Tuzo ya Safal-Cornell. Mji wa Kambare ni diwani iliyotungwa kwa umahiri na ustadi wa aina yake, kuweza kumvutia kila msomaji, awe ni mwanafasihi, mwanaisimu, au mtu wa fani yoyote. Inatokana na uteuzi mzuri wa misamiati inayolandana vina na mizani kiasi ya kuukonga moyo wa msomaji. Muwala, ufundi mkubwa katika kupangilia maneno, ujenzi wa taswira na lugha ya picha, ubobezi katika kumfikirisha msomaji, upana wa dhamira na maudhui yanayopatikana katika tungo zilizomo zinagusia takriban nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Diwani imetumia kwa kiasi kikubwa lahaja za kizanzibari, hasa kipemba. Pia kuna maneno ya Kiswahili asilia yanayoongeza vionjo vya lugha na utamu wa michapo ya mashairi na tungo za Kiswahili cha uswahilini. Maneno magumu yamefafanuliwa maana mwishoni. Itawafaa wapenzi wa mashairi, walimu, wakufunzi, na vikundi vya tamaduni na sanaa.

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Mji Wa kambare”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…