Mkuki Na Nyota Publishers

Vita Vya Kagera

Sh 18,000

Stephen I. Mtemihonda

SKU: 9789987753772 Categories: , Tag:

Kitabu hiki, ‘Vita vya Kagera’, sio tu simulizi ya vita, bali pia inatoa mwanga juu ya nguvu tata za kisiasa na mivutano iliyokuwepo katika jamii ya Afrika Mashariki wakati huo. Kwa maelezo ya kina na ushuhuda wa moja kwa moja, mwandishi wa kitabu hiki, Kanali Mstaafu, Stephen Isaac Mtemihonda ambaye alishiriki pia katika vita hivi akiongoza Kikosi cha 21 cha Brigedi ya 205 anaelezea namna Amin alivyoivamia Tanzania, sababu zake, pamoja na mikakati ya awamu nne iliyowekwa na vikosi vya Tanzania ili kumng’oa. Awamu ya kwanza ilikuwa kuviondoa vikosi vya Amin kutoka kwenye eneo la Kagera, Kaskazini mwa mto Kagera. Awamu ya pili ilikuwa ni kuvivunja vikosi vya jeshi la Amin vilivyokuwa kwenye miji ya Mbarara na Masaka. Awamu ya tatu ilikuwa ni kuikamata miji ya Entebbe na Kampala na pia kuiondoa serikali ya Amin madarakani. Awamu ya nne ambayo ndiyo iliyokuwa ya mwisho, ilitekelezwa baada ya serikali mpya ya Uganda kuingia madarakani. Madhumuni yalikuwa kuwasaka askari wa jeshi la Amin katika maeneo yale ambayo yalikuwa hayajafikiwa na vikosi vya Tanzania. Maeneo hayo yakiwa ni Magharibi, Kaskazini Magharibi, Kaskazini na Mashariki mwa Uganda. Awamu hii ilimalizika rasmi tarehe 4 Juni 1979 baada ya vikosi vya Tanzania kulikalia eneo lote la Jimbo la West Nile, mpakani mwa Congo na Sudan.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Vita Vya Kagera”

Your email address will not be published. Required fields are marked *