Mkuki Na Nyota Publishers

Historia ya Klabu ya Simba

Sh 7,000

Mwina Kaduguda

Hiki ni kitabu cha kwanza chenye historia ya kina ya Simba Sports Club. Kama mpenzi wa soka, hususan mkereketwa wa Simba, utajua chimbuko na undani wake tangu ilipoanzishwa hadi hii leo. Vilevile utaweza kutumia kitabu hiki kama ushahidi katika mabishano na mijadala inayohusiana na klabu.
Utasoma vioja vya soka letu kama vile ushabiki wa kupindukia, vituko na imani za kishirikina, makundi yaliyotia fora, migogoro, mafanikio, picha za matukio mbalimbali, bila kusahau rekodi za mwenendo wa timu na misimamo ya ligi katika historia ya klabu.
Kwa kukisoma kitabu hiki utafahamu pia mambo mengi yanayolizunguka soka la Tanzania, kwani rekodi hizi hazipatikani kwa urahisi na mwandishi ametumia muda mwingi kufanya utafiti na kukusanya taarifa kutoka vyanzo mbalimbali rasmi kama vile maktaba, vitabu, magazeti, nyaraka na kuwahoji wazee wa zamani. Kwa mfano, utajua ni lini soka liliingia na kusambaa nchini katika karne ya 20, mpasuko uliozaa Simba na Yanga na mengine mengi ya kuburudisha, kuelimisha na kusisimua.

Dimensions 270 × 175 mm
Binding

Pages

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Historia ya Klabu ya Simba”

Your email address will not be published. Required fields are marked *