Mkuki Na Nyota Publishers

Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere

Sh 15,000

Peter D.M. Bwimbo

Tarehe 20 Januari 1964, maofisa 15 wa Jeshi la Tanganyika (Tanganyika Army) lililorithiwa kutoka serikali ya kikoloni ya Tanganyika, Colito Barracks (Kambi ya Lugalo) waliongoza maasi ya kijeshi dhidi ya serikali ya Tanganyika. Kikundi kimoja kilikwenda Ikulu kutaka kumlazimisha Rais Nyerere kukubali matakwa yao. Haijulikani ingekuwaje kama kingefanikiwa, na kama Rais Nyerere angeyakataa madai yake. Lolote lingetokea na historia ya Tanzania na ya Afrika ingeathirika vibaya mno.

Kwa ujasiri na ubunifu makini, Peter Bwimbo, aliyekuwa mkuu wa kitengo cha ulinzi wa viongozi, (Presidential Securty Unit) na mlinzi mkuu (Body Guard) wa Rais Nyerere, aliwahamisha Rais Nyerere na Makamo wake Rashid Kawawa, akawapeleka mahali salama, akawaepusha na hatari, pengine ya kuuawa. Hiyo ndiyo iliyoitwa Operesheni Magogoni. Katika kitabu hiki, Mzee Peter Bwimbo, kwa maelezo yake mwenyewe ametoa siri ambayo ni wachache sana waliyoifahamu; haya ndiyo maelezo sahihi ya mbinu alizotumia kuwaokoa viongozi wa nchi.

Kitabu hiki pia ni historia ya Peter Bwimbo, na ya Kitengo cha ulinzi wa viongozi katika Idara ya Usalama wa Taifa. Historia hiyo inaeleza mambo mengi pia kuhusu Tanganyika na Tanzania katika vipindi mbalimbali; jinsi viongozi wa TANU walivyojaribu kuzuia asiwe mlinzi wa Rais kwa sababu alikuwa “jasusi” wa wakoloni katika Special Branch; jinsi Mwalimu alivyoingilia kati na kumaliza fitina hiyo; sifa za kazi ya ulinzi wa Rais (ujasiri, umakini na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na haraka, na uzalendo wa kuwa tayari kujitoa muhanga ili kumlinda) na mengine.

Kutokana na matatizo ya kinidhamu na uadilifu yaliyoikumba Idara ya Usalama wa Taifa, mwaka 1975 Mwalimu aliamua kuwastaafisha viongozi wote wa juu katika Idara ya Usalama wa Taifa, licha ya kuwa alifahamu kuwa Peter Bwimbo hakuwa na dosari yoyote, na hasahasa alikuwa mbele katika kufichua madhambi yaliyokuwa yakitendeka Idarani. Mwaka 1978, alipewa kazi katika Shirika la Reli kuanzisha kitengo cha Usalama, kazi iliyokuwa muhimu sana wakati wa Vita ya Kagera. Mwaka 1985, alipewa Nishani ya Ushupavu (Gallantry Medal) kwa ujasiri wake wakati wa Operation Magogoni na uaminifu wake katika kazi ya Body Guard wa Rais Nyerere.

Dimensions 230 × 150 mm
Binding

Pages

Year published

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere”

Your email address will not be published. Required fields are marked *