“Umesikia George Foreman amerudi ulingoni na kutwaa ubingwa?” Chifu aliuliza.
“Sikusikia tu, nimeona kwenye Televisheni,” Willy Gamba alijibu.
“Basi nataka na wewe urudi ulingoni” Chifu alisema kwa kutabasamu huku akipaka mkate siagi.
Baada ya kufunga ndoa na mpenzi wa maisha yake, Willy Gamba anakuwa mtu mpya asiyetaka kujihusisha tena na purukushani zinazoweza kuhatarisha maisha yake na familia yake. Maamuzi yake hayo yanakosa nguvu pale anapolazimika kuwatolea uvivu viongozi wetu wa Kiafrika ambao wametawaliwa na tamaa ya kubaki kwenye madaraka ili wajilimbikizie utajiri, huku Waafrika wakizidi kudidimia katika dimbwi la umaskini na migogoro ya kisiasa.
Safari hii Willy Gamba anajikuta Rwanda, akitafuta ukweli wa vipi mamilioni ya wananchi waliuawa na wananchi wenzao huku Afrika na dunia wakiangalia bila kutoka msaada wowote.
Uzito wa suala hili unampelekea Willy Gamba kupambana na usaliti na ujahili wa kimataifa ambao uko tayari kuendeleza utawala wa mabavu ili tu maslahi ya watu wachache wenye ubinafsi yaweze kulindwa.
Vijana FM –
Fantastic read!