Mkuki Na Nyota Publishers

Vitimbi vya Mama wa Kambo na Hadithi Nyingine

Sh 15,000

Ally Yusufu Mugenzi

Vitimbi vya Mama wa Kambo, Wivu, Radhi za Wazazi, Rafiki Maluuni, Mchumba Kaka na Adui Mama ni hadithi zinazosawiri jamii alimochipukia mwandishi, au kuishi na kufanya kazi akiwa polisi, mwandishi wa habari na mtangazaji wa redio katika nchi za Tanzania, Rwanda, Burundi, na Uingereza kwa takribani miaka 40. Kitabu hiki ni matokeo ya maombi ya watu wengi waliomsikiliza katika kipindi cha Hadithi na Muziki cha Redio Rwanda katika miaka ya 1980 na 1990. Hadithi hizi pia zimekua zikitumiwa na wakuza mitaala mashuleni na zimewafurahisha wapeniz wengine wa fasihi nje ya shule.

Kuhusu Mwandishi
Ally Yusuf Mugenzi alijiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari Tanzania mwaka 1978. Alipohitimu mwaka 1980, aliajiriwa na Shirika la Habari Tanzania – SHIHATA. Mwaka 1983 aliacha kazi SHIHATA akajiunga na Idhaa ya Kiswahili ya Redio Rwanda alipoajiriwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC – London. Akiwa BBC, alianzisha idhaa ya kukutanisha watu waliotenganishwa na mauaji ya kimbari ya Rwanda. Baaaye ilibadilika na kuwa Idhaa ya Maziwa Makuu. Mwaka 2005 aliteuliwa kuwa mhariri wa idhaa hiyo ambako yuko mpaka sasa.

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Pages

Year published

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Vitimbi vya Mama wa Kambo na Hadithi Nyingine”

Your email address will not be published. Required fields are marked *