Mkuki Na Nyota Publishers

Sankara wa II

Authors: Lubacha Deus

Sh 18,000

Meja Jenerali (MJ), ni kijana anayejulikana mtandaoni kwa kufichua siri za mwenendo wa serikali na jinsi rasilimali zinavyotumika lakini hakuna mtu anayejua nani yupo nyuma ya akaunti hiyo. Maisha yake yanazidi kuwa magumu baada ya kuangukia penzi la Yasmine, binti kipenzi cha Mzee Lumbesa, mtu mwenye nguvu ambaye hataki kuona uhusiano wao ukistawi.

Baada ya Yasmine kuondolewa maishani mwake, MJ anakutana na Salha Kimwana, mtoto wa Waziri Dkt. Nabi, mwenye historia nzito inayoweza kuathiri hata mustakabali wa nchi. Salha anapata faraja kuwa na MJ, lakini MJ ana mipango ya kulipiza kisasi dhidi ya Mzee Lumbesa, na mipango hiyo inamhusisha pia Salha.
Hali inazidi kuwa mbaya, hisia za usaliti, huruma, na vurugu zikizuka, huku siri nzito za familia na siasa zikifichuka, jambo linalopelekea kutanda kwa harufu kali ya damu, kila mmoja akijaribu kulinda alicho nacho.

Hukusu Mwandishi
Lubacha Deus ni mwandishi, mhariri, mtafsiri na mwandishi kivuli kutoka Dar es Salaam. Kazi zake zilizochapishwa na Mkuki na Nyota ni riwaya If She Were Alive iliyoshinda Tuzo ya Burt ya Fasihi ya Kiafrika mwaka 20218, na Parrots of White Feathers (2024), mkusanyiko wa hadithi fupi kumi. Riwaya yake hii, Sankara wa II, imeshinda Tuzo ya Fasihi ya Mwalimu Nyerere mwaka 2024.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Sankara wa II”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…