Riwaya ya kusisimua ya Kiswahili ya A. E. Musiba kutoka mfululizo wa Willy Gamba. Haikuwa kazi yake kujishughulisha na makosa ya jinai, hivyo Willy alishangaa kidogo Chifu alipomwamuru afuatilie tatizo la upungufu wa almasi. Lakini siku hiyo Chifu alivaa sura ya kutisha, na Willy Gamba hakuwa na la kufanya ila kukubali. Kulikuwa na ushahidi kwamba almasi zilizouzwa katika masoko ya nje zilikuwa chache sana kulinganisha na kiasi kilichokuwa kinachimbwa. Kwa nini iko hivyo? Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai imejitahidi bila mafanikio. Askari Polisi Joel amegusa chanzo cha uhalifu, akafa na uhalifu ukaendelea. Chifu anamtuma mpelelezi Jack Mbwile, naye maiti yake inaokotwa ikielea katika Ziwa Victoria. Sasa jambo limekuwa zito na hakuna jinsi, lazima Willy Gamba ahusike.

Kikomo
Author(s): A. E. Musiba, almasi, Kiswahili, riwaya ya kusisimua, uhalifu wa jinai, ujasusi, Willy Gamba, Ziwa Victoria
Sh 8,000
Riwaya ya kusisimua ya Kiswahili ya A. E. Musiba kutoka mfululizo wa Willy Gamba. Almasi za Tanzania zinapotea kimya kimya; Askari Joel na mpelelezi Jack Mbwile wote wamekufa. Willy Gamba lazima ajihusishe, akipambana na mtandao wa uhalifu unaofikia Ziwa Victoria.
| Weight | 0.5 kg |
|---|




Reviews
There are no reviews yet.