Riwaya ya kusisimua ya Kiswahili ya A. E. Musiba kutoka mfululizo wa Willy Gamba. Mpelelezi mashuhuri wa Afrika, Mtanzania Willy Gamba, akiwa likizoni huko Afrika Magharibi jijini Freetown, Sierra Leone, anatumiwa ujumbe wa haraka arudi upesi nchini kwani kumetokea hujuma kubwa. Kutokana na uzalendo wake, hapotezi muda, hima anarejea nchini. Chifu wake anamweleza kuwa shehena kubwa ya silaha za kivita ambazo ni mali ya wapigania uhuru wa kusini mwa Afrika imeibiwa bandarini, katika mazingira ya kutatanisha. Habari hizi zinaleta utata mwingi, baadhi ya nchi zikisema ni njama za Makaburu, na nyingine zikisema ni njama za Tanzania. Katika kiza kinene kinachozunguka suala hili, serikali ya Tanzania inamtuma Willy kuwasaka. Hapo ndipo patashika zinaanza, na jiji la Dar es Salaam linakumbwa na wimbi la msukosuko wa uhaini, usaliti, na mauaji ya kikatili.

Njama
Author(s): A. E. Musiba, Dar es Salaam, Kiswahili, mfululizo, riwaya ya kusisimua, Sierra Leone, ujasusi, Willy Gamba
Sh 10,000
Riwaya ya kusisimua ya Kiswahili ya A. E. Musiba kutoka mfululizo wa Willy Gamba. Silaha za wapigania uhuru wa kusini mwa Afrika zimeibiwa bandarini Dar es Salaam. Willy Gamba anatumwa kuwasaka katika mtandao wa njama za Makaburu, uhaini, na usaliti. Dar es Salaam inakumbwa na wimbi la mauaji ya kikatili.
| Weight | 0.3 kg |
|---|---|
| Dimensions | 195 × 130 mm |
| Binding | |
| Pages | |
| Year published |




Fakih Mzee –
napenda story za hyu mwamba