Mkuki Na Nyota Publishers

Kusadikika

Author(s): classic, fasihi ya Kiswahili, haki, Kiswahili, mshairi wa taifa, riwaya, Shaaban Robert, ufalme wa kubuni

Sh 7,000

Riwaya maarufu ya kifalsafa ya Shaaban Robert, iliyochapishwa kwa mara ya kwanza wakati wa ukoloni. Hadithi ya nchi ya kubuni ambapo dhuluma zinatendwa dhidi ya kanuni za haki, sheria, na ubinadamu. Kutoka kwa mshairi wa taifa wa Kiswahili, mwandishi maarufu kushinda wote katika jamii za Waswahili.

Riwaya maarufu ya Sheikh Shaaban Robert iliyochapishwa kwa mara ya kwanza wakati wa ukoloni. Ni hadithi ya kifalsafa ya nchi au ufalme wa kubuni ambapo dhuluma zinatendwa dhidi ya kila kanuni ya haki, sheria, na ubinadamu. Kutoka kwa bingwa wa lugha na utamaduni wa Kiswahili. Shaaban Robert ni mwandishi maarufu kushinda wote katika jamii za Waswahili kote Afrika ya Mashariki na Kati. Kwa zaidi ya miaka kumi na tano, vitabu vyake havikupatikana Tanzania kwa sababu kampuni ya kigeni iliyovichapisha iliacha kuvichapisha kutokana na hali mbaya ya uchumi. Athari ya kupotea kwa vitabu vyake ni kwamba Watanzania wengi hawamjui mwandishi huyu maarufu. Kwa kuvichapisha tena vitabu vya Marehemu Sheikh Shaaban Robert, Watanzania, hasa vijana, wanakaribishwa tena kuvisoma.

Dimensions 206 × 137 mm
Binding

Pages

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Kusadikika”

Your email address will not be published. Required fields are marked *