Riwaya ya kwanza ya Mbwana Kidato, iliyoshinda Tuzo ya Safal-Cornell, inayotokana na tukio la kweli alilolisoma alipokuwa akipitia majarida mbalimbali ya Tanzania kwenye mtandao. Alikutana na habari ya kuhuzunisha ya msichana mwenye ulemavu wa ngozi aliyekatwa viungo vya mwili wake. Hii ni kazi ya kufikirika, yenye kuelimisha, kuakisi maisha yetu, na kutuuliza maswali juu ya utu wetu. Je, miongoni mwetu kuna wengine wana utu wenye thamani zaidi ya utu wa wengine? Kama kuna kipimo cha utu, huo utu unapimwa na kipimo cha aina gani? Je, kipimo hicho ni maumbile yetu au ni tabia zetu? Ama ni vitu vinavyotuzunguka? Mwandishi anajaribu kuuliza haya maswali kupitia mhusika mkuu wa riwaya, Sinaubi. Mbwana Kidato ni mtengenezaji wa vipindi vya runinga na filamu, aliyepata elimu yake Uingereza katika nyanja za uandishi, utengenezaji, na uhariri wa picha, na ameshawahi kufanya kazi na Shirika la Utangazaji la Tanzania.

Sinaubi
Author(s): albinism, filamu, Kiswahili, Mbwana Kidato, riwaya, Safal-Cornell, Uingereza, ulemavu wa ngozi
Sh 30,000
Riwaya ya kwanza ya Mbwana Kidato, mshindi wa Tuzo ya Safal-Cornell. Inatokana na tukio la kweli la msichana mwenye ulemavu wa ngozi aliyekatwa viungo vya mwili wake. Maswali ya thamani ya utu yanajadiliwa kupitia mhusika Sinaubi. Mwandishi pia ni mtengenezaji wa filamu.
| Dimensions | 195 × 130 mm |
|---|---|
| Binding |
You may also like…
-

The African Epic Controversy
Sh 45,000




Reviews
There are no reviews yet.