Mkuki Na Nyota Publishers

Penzi la Damu

Author(s): Anna Samwel Manyanza, Kiswahili, Mabati-Cornell, Malaika, mapenzi, riwaya, Safal-Cornell, tuzo ya fasihi

Sh 18,000

Riwaya ya kwanza ya Anna Samwel Manyanza, iliyoshinda Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika. Malaika anasafiri ughaibuni kwa masomo; mpenzi wake Ben anaahidi kumsubiri. Utengano, majaribu, na vishawishi vinatishia penzi lao. Related: Row 311 (author’s second novel).

Riwaya ya kwanza ya Anna Samwel Manyanza, iliyoshinda Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika. Mstahamilivu hula mbivu, mtaka cha uvunguni sharti ainame, na mchumia juani hulia kivulini; ni machache ya maadili yamuongozayo binti Malaika katika safari yake ya kutimiza ndoto zake. Kujiendeleza kielimu ndiyo ndoto yake kuu. Kwa vile Mungu hamtupi mja wake, anabahatika kwenda ughaibuni kitaaluma. Ni safari inayomtenganisha na mpenzi wake Ben. Lakini Ben anaahidi kumsubiri hadi afuzu masomo yake. Katika kipindi hiki cha utengano, dunia inawapangia mambo mengine kabisa; ni utengano unaotishia kulisumu penzi lao. Majaribu hayeshi, vishawishi ni vingi. Penzi lao linayumba, linatishia kudumbukia kwenye dimbwi la damu. Lakini Malaika haliachii penzi lake kwa Ben, analipigania kishujaa. Ben pia anaingia vitani kulipigania penzi la Malaika. Je, watashinda vita hivi vya kimapenzi? Riwaya yake ya pili ni Faradhi ya Moyo (Row 311).

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Penzi la Damu”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…