Sauti dhaifu ya kilio cha mwanamke ilinifikia pale nilipokuwa nimesimama karibu na vikubwa vilivyoshonana mbele yangu. “Hivi ni sauti ya binadamu kweli au ni mlio wa mnyama fulani”? Nilijiuliza swali hilo ingawa sauti ile niliyoisikia ilifanana sana na kilio cha mwanamke ambaye yuko katika maumivu makali. Hali fulani ya woga ilianza kuniingia polepole. Baada ya kuanza kupatwa na woga niliamua kumfuata bibi yangu ambaye nilimwacha akiendelea kukata kunu nyuma ya vichaka vingine vilivyokuwa kushoto kwangu.
Baada ya kutembea kwa hatua zisizozidi kumi nilimwona bibi akinifuata. Hapo niliamua kusimama kumsubiri ili nimwulize juu ya ile sauti niliyosikia. “Nimesikia sauti kama ya mtu ambaye alilia kwa muda mrefu na mwisho akapoteza nguvu”. Bibi yangu aliieleza hivyo kabla ya mimi kumweleza. “Hata mimi niliisikia ile sauti, tena inaelekea ni sauti ya mwanmke. Hivi unavyoniona ndio nimeamua kutofuata tena hizo kuni, maana nimeanza kuogopa.”








Reviews
There are no reviews yet.