Tafsiri ya Kiswahili ya riwaya Paradise ya Abdulrazak Gurnah, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi ya mwaka 2021. Hii ni tafsiri ya kwanza ya riwaya za Gurnah katika lugha yoyote ya Kiafrika. Mtafsiri ni Dkt. Ida Hadjivayanis, Mhadhiri Mwandamizi wa Masomo ya Kiswahili SOAS, Chuo Kikuu cha London. Mzaliwa wa Afrika ya Mashariki, Yusuf anaondoka kwao kwa ghafla akiwa na umri wa miaka kumi na mbili. Haimjii hata kwa sekunde moja kwamba atakuwa mbali na wazazi wake kwa muda mrefu, wala hafikirii kuuliza atarudi lini. Yusuf anaamini kuwa anamsindikiza Ami Aziz, lakini ukweli ni kwamba ami yake ni mfanyabiashara tajiri mkubwa, na Yusuf amewekwa rehani ili kulipia madeni ya baba yake. Yusuf anasafiri katika miji na vitongoji vingi, anakutana na watu wa kila namna, na anabalehe katika dunia inayobadilika kwa kasi kutokana na kuingia kwa ukoloni na udhalimu wake. Gurnah ni Profesa wa Masomo ya Kiingereza na Fasihi za Kikoloni katika Chuo Kikuu cha Kent.

Peponi
Author(s): Abdulrazak Gurnah, Ida Hadjivayanis, Kiswahili, Nobel Prize, Paradise, Peponi, tafsiri, Zanzibar
Rated 5.00 out of 5 based on 1 customer rating
(1 customer review)
Sh 22,000
Tafsiri ya kwanza ya Kiswahili (na ya kwanza katika lugha yoyote ya Kiafrika) ya riwaya Paradise ya Abdulrazak Gurnah, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi 2021. Imetafsiriwa na Dkt. Ida Hadjivayanis wa SOAS. Yusuf, mtoto wa miaka kumi na mbili, amewekwa rehani ili kulipia madeni ya baba yake, na safari yake inamuonyesha Afrika inayobadilika chini ya ukoloni.
ISBN: 9789987449866
Category: Fiction
Tags: Abdulrazak Gurnah, Ida Hadjivayanis, Kiswahili, Nobel Prize, Paradise, Peponi, tafsiri, Zanzibar
| Weight | 0.4 kg |
|---|
1 review for Peponi
Add a reviewCancel Reply
Related products
-

Remembering the Revolution in Zanzibar
Sh 30,000 -

Mji Wa kambare
Sh 15,000 -

Colombian Roulette
Sh 25,000 -

Dhulma
Sh 40,000
Aloyce shulla –
I love it