Mchezo wa saba katika mfululizo wa vitabu vya michezo ya kuigiza kutoka Tanzania Publishing House. Michezo hii imeendelea kuburudisha na kuelimisha wasomaji wa rika zote tangu ilipochapishwa kwa mara ya kwanza, na imechaguliwa kufundishia lugha na drama mashuleni. Kijiji Chetu ni mchezo wa kuigiza kuhusu kijiji chenye uongozi mbaya. Kama inavyoeleweka, ngao ya wakulima ni ushirika. Wakati ushirika huo haupo, maendeleo nayo hayapatikani au yatakuwa mashakani. Mchezo unamulika baadhi ya sababu za msingi zinazozuia kukua kwa ushirika, zikiwemo ubinafsi, ulaghai, uzembe, na ufisadi. Mwandishi Bwana Ngalimecha Ngahyoma ni mkurugenzi wa vipindi maalum wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), na ni mwandishi pia wa mchezo mwingine uliochapishwa na Tanzania Publishing House uitwao Huka.

Kijiji Chetu
Author(s): Kiswahili, mchezo wa kuigiza, Ngalimecha Ngahyoma, shule, tamthilia, Tanzania Publishing House, ufisadi, ushirika
Sh 6,000
Tamthilia ya Kiswahili ya Ngalimecha Ngahyoma, mchezo wa saba katika mfululizo wa Tanzania Publishing House. Inamulika sababu zinazozuia ushirika wa wakulima vijijini: ubinafsi, ulaghai, uzembe, na ufisadi. Imechaguliwa kufundishia lugha na drama mashuleni Tanzania.
Available on backorder




Reviews
There are no reviews yet.