Kamusi ya kwanza ya lugha ya Kiswahili inayoweka pamoja tafsiri ya dhana mbalimbali, majina mbalimbali ya Wakristo, na desturi za makanisa ya Kikristo. Mwandishi Jordan Nyenyembe amefuatilia kwa umahiri mkubwa na kufanikiwa kukusanya vitomeo vinavyowakilisha madhehebu mbalimbali ya Kikristo. Kuna vidahizo vinavyotumiwa zaidi na dhehebu moja kuliko lingine, lakini mwandishi ameviweka pamoja ili kuondoa umadhehebu na kujenga umoja wa Ukristo. Ni ukweli usiopingika kuwa waamini wengi hawaelewi misamiati na istilahi nyingi za dini zao. Kwa msaada wa kamusi hii, msomaji atafaidi maarifa ya maana na matumizi ya maneno, si tu ya dhehebu lake bali Ukristo kwa ujumla. Marejeleo muhimu kwa viongozi wa kanisa, walimu wa dini, na wasomaji wa kawaida wanaotaka kuelewa istilahi za Kikristo katika lugha ya Kiswahili.

Kamusi ya Ukristo
Author(s): dini, Jordan Nyenyembe, kamusi, Kiswahili, madhehebu, makanisa, marejeleo, Ukristo
Sh 15,000
Kamusi ya kwanza ya Kiswahili ya Ukristo, iliyoandaliwa na Jordan Nyenyembe. Inakusanya dhana, majina, na desturi za makanisa mbalimbali ya Kikristo, ikiweka pamoja vidahizo vinavyotofautisha madhehebu ili kujenga uelewa wa pamoja. Marejeleo kwa viongozi wa kanisa, walimu wa dini, na wasomaji wanaotaka kufahamu istilahi za Ukristo kwa Kiswahili.




Reviews
There are no reviews yet.