Mkuki Na Nyota Publishers

Uswahilini

Sh 20,000

Ally Bakari Mchanyato

Mbali na dhana iliyotawala kwenye jamii kwamba Uswahilini ni sehemu iliyosheheni vituko na maovu yaliyokubuhu, na misemo iliyoe nea kuwa Waswahili ni watu wasioishiwa visa na mikasa, mwandishi wa diwani hii ameukumbatia Uswahili kwa kuimulika hali halisi ya maisha yaliyopo na mambo yatokeayo kuanzia mapenzi, elimu na mbinu za kuitafuta, siasa, dini na nasaha zake njema, mbinu za kujik wamua kiuchumi, malezi pamoja na haki za wanawake. Waswahili si watu wa kubezwa na kushushwa hadhi kama ambavyo wengi wamekuwa wakiichulia jamii ya Waswahili na Waswahili wenyewe. Hakika Uswahilini kuna mengi mazuri ya kuwasaidia Waswahili na jamii zinazochangamana na Waswahili, kinyume na yale yanayosemwa kuwa uswahilini kuna vituko.

Kuhusu Mwandishi

Ally Bakari mchanyato ni mzaliwa was Ilala jijini Dar es Salaam na ni mjasiriamali. Alianza kuandika mwaka 1998 na shairi lake la kwanza lilihusu kifo cha baba yake mzazi, na baadaye alianza kuandika hadithi fupi zilizochapishwa kwenye magazeti ya Uwazi na Alasiri. Baadaye alianza kuandika tenzi kwa ajili ya maharusi, kwenye mahafali ya shule na kwenye vyuo vya dini ya kiislamu. Mwaka 2023 alikuwa mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Safal Cornell ya Fasihi ya Afrika katika kipengele cha ushairi.

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Uswahilini”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…