Haki, amani na maendeleo ni vitu muhimu katika maisha ya binadamu. Binadamu hawezi kupata maendeleo ya kweli kama hakuna haki; aidha maendeleo hayapatikani kama hakuna amani; nayo amani haitakuwepo kama hakuna haki. Mambo yote hayo matatu yanategemeana. Pamoja na kutegemeana huko, haki inachukua nafasi ya kwanza kwani ndiyo inayozaa hayo mengine mawili. Miongoni mwa mambo mengine, kitabu hiki kinajadili mfumo wa utoaji haki nchini Tanzania, mahakama za Tanzania, hali halisi ndani yake, na nini kifanyike ili kurekebisha mambo. Mwandishi, Mh. Jaji Steven James Bwana, amekuwa mtumishi wa Mahakama tangu mwaka 1975, na mwaka 2008 aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Hiki ni kitabu chake cha tisa.

Haki, Amani na Maendeleo
Author(s): amani, falsafa ya sheria, haki, maendeleo, Mahakama, sheria ya Tanzania, Steven Bwana, Swahili legal writing
Sh 9,000
Haki, amani na maendeleo ni vitu vinavyotegemeana, na haki ndiyo msingi inayozaa mengine mawili. Jaji Steven James Bwana wa Mahakama ya Rufani Tanzania, mtumishi wa Mahakama tangu mwaka 1975 na mwandishi wa vitabu tisa, anachambua mfumo wa utoaji haki nchini Tanzania, hali halisi ndani yake, na nini kifanyike kurekebisha mambo.
| Weight | 0.1 kg |
|---|---|
| Binding |




Reviews
There are no reviews yet.