Mkuki Na Nyota Publishers

Wimbo wa Hatima

Sh 22,000

Isaac Ndolo

Ndolo Kamala, kijana msomi na mtoto wa Chifu Uvunyu wa Matani, ambaye pia ni Mrithi pekee wa Kiti cha baba yake, anaungana na Elude, binti jasusi kutoka Uingereza mzaliwa wa Ufaransa katika jukumu lake la kuhakikisha anaharibu mpango wa Ujerumani wa kuzalisha silaha kali ya Kibiolojia ya kufubaza ubongo ama utambuzi wa binadamu (Pathojeni ya Upako) nchini Tanganyika, silaha ambayo ingetumiwa na Ujerumani dhidi ya maadui zake wote wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia. Hata hivyo wakiwa katikati ya jukumu lao, Kamala na Elude wanajikuta wakianguka ndani ya penzi, huku tofauti zao za rangi na mila zikiwafanya wote wawili waanze kuzitafakari hatima zao…

Kuhusu Mwandishi

Isaac Ndolo ni mwandishi wa lugha mbili, Kiswahili na Kiingereza. Ni mhitimu wa Isimu mwenye shahada ya uzamili katika Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Moi, Kenya. Mnamo mwaka 2021, alichapisha riwaya yake ya kwanza kwa Kiingereza iliyopewa jina The Song of Destiny. Baadaye, alitafsiri kazi hiyo kwa Kiswahili na kuibuka mshindi wa Tuzo ya Kiswahili ya Salfal Cornell katika jaribio lake la kwanza.

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Wimbo wa Hatima”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…