Mkuki Na Nyota Publishers

Wimbo wa Hatima

Author(s): Isaac Ndolo, Kamala, Kiswahili, riwaya, Safal-Cornell, Tanganyika, Ujerumani, Vita vya Kwanza vya Dunia

Sh 15,000

Riwaya ya Kiswahili ya Isaac Ndolo, mshindi wa Tuzo ya Safal-Cornell (tafsiri yake mwenyewe ya The Song of Destiny, 2021). Kamala wa Tanganyika na Elude, jasusi wa Uingereza, wanapambana na mpango wa silaha ya kibiolojia ya Ujerumani wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia, huku wakiingia kwenye penzi.

Riwaya ya Kiswahili iliyoandikwa na Isaac Ndolo, mshindi wa Tuzo ya Kiswahili ya Safal-Cornell ya Fasihi ya Afrika. Ndolo Kamala, kijana msomi na mtoto wa Chifu Uvunyu wa Matani, ambaye pia ni mrithi pekee wa kiti cha baba yake, anaungana na Elude, binti jasusi kutoka Uingereza mzaliwa wa Ufaransa, katika jukumu la kuhakikisha wanaharibu mpango wa Ujerumani wa kuzalisha silaha kali ya kibiolojia ya kufubaza ubongo na utambuzi wa binadamu (Pathojeni ya Upako) nchini Tanganyika. Silaha hii ingetumiwa na Ujerumani dhidi ya maadui zake wote wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia. Hata hivyo, wakiwa katikati ya jukumu lao, Kamala na Elude wanajikuta wakianguka ndani ya penzi, na tofauti zao za rangi na mila zinawafanya wote wawili waanze kutafakari hatima zao. Isaac Ndolo ni mwandishi wa lugha mbili, Kiswahili na Kiingereza, mhitimu wa Isimu mwenye Shahada ya Uzamili katika Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Moi, Kenya. Riwaya hii ni tafsiri yake ya riwaya yake ya The Song of Destiny (2021).

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Wimbo wa Hatima”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…