Mkuki Na Nyota Publishers

Mirathi ya Hatari

Sh 8,000

C.G. Mungóngó

SKU: 9789976102451 Categories: , , Tag:

Gusto, kijana mdogo wa shule, hakurithi mali ya marehemu baba yake tu, bali pia amerithi tunguri zake, madaraka yake ya kiwanga na mlolongo mzima wa visa, visasi na vinyongo vya baba yake. Urithi huu, unamtoa Gusto katika ulimwengu wa wachawi. Hatimaye, baada ya kupambana na vitimbi, hasara na mikasa ya kutisha, inambidi Gusto akate shauri kati ya kuyatekeleza matakwa ya marehemu baba yake na kuyatimiza matakwa ya dhamiri yake binafsi na ya jumuiya yake inayotafuta maendeleo ya kisasa. Mvutano unaotokea, unakiuka uwezo wake alioupata shuleni, na kutisha kumrarua vipande vipande…

Hiki ni kisa cha kutisha na kutaharakisha, kinachotuingiza katika undani wa uganga wa uchawi na mazingaombwe, na hatimaye kutuacha tukijiuliza kama kweli mambo hayo yanayo manufaa yoyote kwa jamii yetu au ni doa na mirathi ya hatari tu katika utamaduni wetu.

Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Mirathi ya Hatari”

Your email address will not be published. Required fields are marked *