Mkuki Na Nyota Publishers

Tusiogope

Author(s): Asia Kasuwi Kapande, kilimo, Kiswahili, Shirika la Uchumi wa Nyumbani, Tanzania, tawasifu, wanawake, watoto wasiojiweza

Sh 18,000

Tawasifu ya Kiswahili ya Bi. Asia Kasuwi Kapande, mwanamke Mtanzania aliyepambana katika sekta ya kilimo, akashirikia kuanzisha Shirika la Uchumi wa Nyumbani Tanzania, na akasaidia watoto wasiojiweza. Jozi ya kitabu cha Kiingereza katika Row 385 (Let’s Fear Not).

Tawasifu ya Kiswahili ya mwanamke jasiri Bi. Asia Kasuwi Kapande aliyeamini kuwa anaweza kufikia malengo yake na aliyeona fursa pale wengine walipoona changamoto tu. Alijua kuzitumia vizuri fursa hizo, siyo kwa manufaa yake binafsi tu, bali kwa kuwatunuku wengine maarifa, ujuzi, na rasilimali za fedha kwa kadiri ya uwezo wake. Bi. Kapande anaelezea kwa uwazi maisha yake ya shule, familia, ajira, kushiriki kwake katika kuanzisha Shirika la Uchumi wa Nyumbani Tanzania na katika siasa, nafasi za usimamizi katika vyuo mbalimbali vya kilimo nchini, na shughuli za kiuchumi na kijamii baada ya kustaafu. Alikuwa na bahati ya kupata elimu ya juu ndani na nje ya nchi, lakini licha ya hivyo haikuwa kawaida kwa msichana kuajiriwa katika sekta ya kilimo kutokana na vikwazo vijana wa kike walivyowekewa. Hakusita; alikazana kutafuta maarifa, na hayo ameyapa nafasi kubwa katika kitabu hiki. Anaeleza jinsi alivyomudu kazi zake kwa kutatua changamoto mbalimbali katika kilimo na ufugaji, na mchango wake katika elimu na kusaidia watoto wasiojiweza. Jozi ya kitabu cha Kiingereza katika Row 385 (Let’s Fear Not).

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Tusiogope”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…