Mkuki Na Nyota Publishers

Tendehogo

Author(s): Afrika Mashariki, biashara ya utumwa, Kiswahili, kitabu cha shule, S. Edwin Semzaba, tamthilia, Tanzania Publishing House, utumwa

Sh 6,000

Tamthilia ya Kiswahili ya S. Edwin Semzaba kuhusu mfumo wa utumwa na athari zake kwa walioathirika. Mchezo wa kumi na saba katika mfululizo wa tamthilia za Tanzania Publishing House/Mkuki na Nyota. Umechaguliwa kufundishia drama na Kiswahili mashuleni. Unaonyesha ujasiri, mivutano, usaliti, na migongano.

Tamthilia ya Kiswahili iliyoandikwa na S. Edwin Semzaba. Huu ni mchezo wa kumi na saba katika mfululizo wa vitabu vya michezo ya kuigiza kutoka Mkuki na Nyota. Michezo hii imeendelea kuburudisha na kuelimisha wasomaji wa rika zote tangu ilipochapishwa kwa mara ya kwanza. Kitabu hiki kimechaguliwa kufundishia lugha na drama mashuleni. Tendehogo ni tamthilia inayohusu mfumo wa utumwa na athari zake kwa wale waliokumbwa nao. Mchezo unaakisi yaliyotokea katika kipindi cha biashara ya utumwa Afrika ya Mashariki. Mchezo unaonyesha ujasiri, mivutano, usaliti, na migawanyiko miongoni mwa watumwa. Vilevile unaonyesha mapambano na migongano iliyoibuka kati ya watumwa na wamiliki wao hadi kupelekea kilele ambacho hakika kitakusisimua. Mchezo unamsaidia mwanafunzi wa Kiswahili na drama kuelewa historia ngumu ya biashara ya utumwa katika mazingira ya fasihi.

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Tendehogo”

Your email address will not be published. Required fields are marked *