Tafsiri ya Kiswahili ya tamthilia mbili za Kifaransa: Le Roi s’amuse ya Victor Hugo (1802-1855) na Les règles du savoir vivre dans la société moderne ya Jean-Luc Lagarce (1957-1995). Mtafsiri ni Profesa Marcel Kalunga Mwela-Ubi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na tafsiri hizi zilishinda tuzo katika mashindano ya kutafsiri tamthilia za Kifaransa katika Kiswahili. Tafsiri zimefanyika katika Kiswahili cha Congo (Kingwana), mojawapo ya lahaja za Kiswahili inayozungumzwa na pengine idadi ya pili au ya tatu kubwa ya watumiaji wa Kiswahili nje ya Tanzania. Katika Michezo ya Mfalme, Hugo anaeleza hadithi ya Mfalme mpenda wanawake, na Triboulet, mtumwa wake mwenye kilema, ambaye hatimaye anatafuta njia ya kulipiza kisasi.
Swahili translations of two French plays: Victor Hugo’s Le Roi s’amuse and Jean-Luc Lagarce’s Les règles du savoir vivre dans la société moderne, by Professor Marcel Kalunga Mwela-Ubi of Lubumbashi and Kalemie Universities, DRC. Rendered in Congolese Swahili (Kingwana). Internationally distributed by African Books Collective.





Reviews
There are no reviews yet.