Kuanzisha biashara yenye mafanikio inahitaji zaidi ya mtaji, bidhaa za kuuza na dhamira ya kupata faida. Inahitaji sifa fulani na mikakati mahsusi iliyowahi kufikiwa na wajasiriamali waliotangulia miaka kwa miaka. Waandishi na wataalamu wa biashara wamekusanya taarifa na kuzipembua hadi kuwa kilele cha maarifa unayoweza kuyatumia kuanzisha au kuendeleza biashara yako uliyonayo kwa ngazi ya juu zaidi.
Stadi za Ujasiriamali:
Ni Kitabu kinachoeleza mikakati ya mafanikio kwenye soko lenye ushindani. Kimebeba mzigo huu wa maarifa katika lugha rahisi kueleweka iliyonogeshwa kwa vionjo vya mifano halisi.
Jifunze jinsi ya:
Kujitathmini mwenyewe ili kujua kama ujasiriamali ni fani sahihi kwako.
Kuchagua biashara sahihi na mfumo wa uendeshaji unaokufaa.
Kutambua na kuwekeza katika mawazo mazuri ya biashara.
Kuanzisha na kuendesha biashara yako kwa ufanisi.
Kuwatangulia washindani wako kupitia maarifa & teknolojia.
Kuepuka matumizi na gharama zisizo za lazima zinazodidimiza makampuni mengi.
Kutumia njia rahisi za kupata masoko kwa bidhaa zako.
Kufikiri kwa mapana na kuanza taratibu ukiweka akili yako yote kwenye biashara yako
Kuepuka makosa yaliyozoeleka yanayopelekea biashara kuporomoka.
Kuhusu Mwandishi
Murori Kiunga ni mjasiriamali, mkufunzi na mwandishi mahiri kutoka Nairobi, Kenya. Vitabu vyake maarufu vinajumuisha:
The Art of Entrepreneurship (ambacho hii ni tafsiri yake ya kiswahili)
The Winning Character: Succeeding Where Others Fail, The 7 Pillars of Financial Success, The Entrepreneurial Journey.
From Employmemnt to Business and Common Reasons why start-up Business Fail and what you can do about
Reviews
There are no reviews yet.