Mkuki Na Nyota Publishers

Mamangu Nipe Wosia

Author(s): diwani, Kiswahili, malezi, mama, Safal-Cornell 2022/23, Salum Makamba, ushairi, UWARIDI

Sh 12,000

Diwani ya ushairi ya Kiswahili ya Salum Makamba, mshindi wa Tuzo ya Kiswahili ya Safal-Cornell ya Fasihi ya Afrika 2022/23. Mafunzo kwa vijana kupitia neno mama, yaliyoenea kuchunguza siasa, mazingira, maisha na kifo, uanamajumui, na mapenzi. Mwandishi chipukizi wa UWARIDI.

ISBN: 9789987082209 Category: Tags: , , , , , , ,

Diwani ya ushairi ya Kiswahili iliyoandikwa na Salum Makamba, mshindi wa Tuzo ya Kiswahili ya Safal-Cornell ya Fasihi ya Afrika mwaka 2022/23. Mamangu Nipe Wosia ni diwani inayotoa mafunzo na maonyo kwa vijana ili waweze kwenda katika njia zifaazo maishani. Maudhui yake yaliyobebwa na neno mama yana nguvu ya uzazi na ulezi ndani yake, yenye uwezo wa kumuongoza hata kijana yatima au yule aliyekosa mausia yaliyo mema. Fauka ya hayo, si diwani iliyojikunyata mithili ya kifaurongo; kwani ikiachana na masuala ya malezi, imeangazia pia siasa, uhifadhi wa mazingira, maisha na kifo, uanamajumui, mapenzi, na masuala mengine yaliyojadiliwa kwa mitindo tofautitofauti iliyosukwa kwa ufundi wa hali ya juu. Salum Makamba ni mwandishi chipukizi kutoka Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira (UWARIDI) nchini Tanzania.

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Mamangu Nipe Wosia”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…