Uswahilini kwetu kuna semi nyingi za wahenga na wavyele zinazohimiza na kusisitiza mambo kufanywa kwa juhudi na ufanisi ili kufanikiwa. Hili linaweza kuthibitika katika mtano wa methali isemayo “kula uhondo kwataka matendo, asiye na matendo hula uvundo” ikiwa na maana mafanikio hayapatikani burebure bila kufanyika kwa juhudi. Hakuna kitu cha thamani kinachoweza kupatikana bila gharama, na gharama si tu pesa bali inaweza kuwa nguvu, muda, afya sambamba na kujitoa kikwelikweli katika kupambania jambo kwa imani, utiifu, subira na juhudi. Diwani ya Bure Ghali inaeleza hilo kwa beti na si hilo tu pia inagusa nyonyo na hisia za watu kwa kueleza furaha na huzuni zetu katika kazi, mapenzi, uongozi, utajiri, umasikini na mamoo kadha wa kadha.
KUHUSU MWANDISHI
Bashiru Abdallah ni mshairi aliyewahi kushinda Tuzo ya Pan African Writers Association (PAWA) baada ya diwani ya Wino wa Dhahabu kuwa diwani bora kwa upande wa lugha ya Kiswahili mwaka 2021. Pia mswada huo uliingia kwenye orodha fupi ya Tuzo ya Kiswahili ya Mabati Cornell wakati huo mwaka 2018.
Aidha, amewahi kushika natası ya pili katıka Tuzo ya Ushairi ya Ebrahim Hussein (TUEHU) kwa miaka miwili mtawalia, 2018 na 2019. Kabla ya diwani hii, ameshachapisha diwani 5 ambazo ni Hatma Yangu, Wino wa Dhahabu, Neni Kiamboni, Harufu ya Nuni na Uwapi Mwanangu? Halikadhalika, kuna diwani nyingine 2 akiwa na watunzi wengine ambazo ni Ndimi Zenye Ncha na Ahadi Iliyotimizwa. Diwani hii imeshika Nafasi ya Kwanza katika Tuzo ya Kiswahili ya Safal ya Fasihi ya Afrika 2025.





Reviews
There are no reviews yet.