Mkuki Na Nyota Publishers

Kifaurongo

Author(s): Christopher Bundala Budebah, diwani, Kiswahili, Mabati-Cornell, Maswa, Safal-Cornell, TUKI, ushairi

Sh 10,000

Diwani ya ushairi ya Kiswahili ya Christopher Bundala Budebah, mshindi wa Tuzo ya Safal-Cornell na ya Jubilei ya miaka 75 ya TUKI. Mashairi yanayodokeza ukoloni mamboleo, usaliti, mila potofu, haki za mtoto, UKIMWI, rushwa, na uwajibikaji. Budebah ni mhitimu wa M.A. Kiswahili.

Diwani ya ushairi ya Kiswahili iliyoandikwa na Christopher Bundala Budebah, mshindi wa Tuzo ya Safal-Cornell na ya Jubilei ya miaka 75 ya TUKI. Diwani hii ina mashairi mesto yatakayomwezesha msomaji kujitanua bila ukinzani wa uguni na usiguni, usasa na umapokeo, hivyo azingatie fani, maudhui, na muktadha. Dhana zilizodokezwa ni ukoloni mamboleo, usaliti, mila potofu, ukatili, unyanyasaji wa kijinsia, haki za mtoto, UKIMWI, rushwa, kiwi ya akili, uwajibikaji, na nyinginezo. Budebah alizaliwa mwaka 1956 huko Maswa, Simiyu. Ni mhitimu wa M.A. Kiswahili, Stashahada ya Uzamili ya Ualimu, Shahada ya Kwanza ya Sanaa za Maonyesho, na Cheti cha Sanaa za Maonyesho. Ameshiriki makongamano ya Kiswahili ya kimataifa huko Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda, Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya, na Chuo Kikuu cha Mtakatifu John, Dodoma. Ametoa makala katika jarida la Kiswahili la Kioo cha Lugha.

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Kifaurongo”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…