Mkuki Na Nyota Publishers

Mamangu Nipe Wosia

Sh 15,000

Salum Makamba

Mamangu Nipe Wosia ni diwani inayotoa mafunzo na maonyo kwa vijana ili waweze kwenda katika njia zifaazo maishani. Maudhui yake yaliyobebwa na neno ‘mama’ yana nguvu ya uzazi na ulezi ndani yake iliyo na uwezo wa kumwongoza hata kijana yatima au yule aliyekosa mausia yaliyo mema. Fauka ya hayo, si diwani iliyojikunyata mithili ya kifaurongo, kwani ukiachana na masuala ya malezi, imeangazia pia siasa, uhifadhi wa mazingira, maisha na kifo, uanamajumui, mapenzi na masuala mengine kadha wa kadha ambayo yamejadiliwa kwa mitindo tafautitafauti iliyosukwa kwa ufundi wa hali ya juu.

Kuhusu Mwandishi

Salum Makamba ni mwandishi chipukizi kutoka Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira (UWARIDI) nchini Tanzania. Mbali na riwaya, huandika hadithi fupi, mashairi, tamthiliya, insha na makala juu ya masuala mbalimbali ya kijamii. Ana uzoefu katika nidhamu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma kutoka Mtandao wa Wanahabari Vijana na Watoto jijini Mwanza (MYCN), ana Shahada ya Udaktari wa Binadamu, vilevile ni Mshindi wa Tuzo ya Kiswahili ya Safal Cornell ya Fasihi ya Afrika mwaka 2022/23. Ni mwandishi ambaye mbali na kuburudisha, kalamu yake anaielekeza katika kufunza, kuonya, kuelimisha na kuikumbusha jamii juu ya masuala mbalimbali iliyoyapiga teke na kuyapuuza au isiyoyasema sana kutokana na hofu au kutokujua.

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Mamangu Nipe Wosia”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…