Mkuki Na Nyota Publishers

Maisha ya Mchagga Hapa Duniani na Ahera

Sh 10,000

Author(s): Petro Itosi Marealle

Out of stock

Maisha ya Mchagga Hapa Duniani na Ahera

Mangi Petro Itosi Marealle, aliyekuwa Mangi Mwitori wa Vunjo, amewafanyia kabila la Wachagga na wazao wa baadaye, kazi ya maana sana kwa kuandika kitabu hiki juu ya desturi za Wachagga kabla hazijatoweka na kupotea. Alijitolea miaka mingi kujifunza kwa uangalifu mila na desturi hizi, na alipata mashaka katika kutafuta njia ya kukichapa kitabu hiki. Ninafurahi kusema amekwisha pata njia. Natumaini kitabu hiki hakitapendwa na Mchagga tu, lakini kila mmoja atakaye kujifunza maendeleo ya Wana-Adamu, na natumaini kitaamsha Wa-Africa wa makabila mengine kutunga habari za namna hii za watu wao.

Mwandishi wa kitabu hiki, Marehemu Mangi Petro Itosi Marealle, alikuwa Mangi wa Marangu kuanzia mwaka 1931 hadi 1946, na ‘Mangi Mwitori’ wa Vunjo hadi mwaka 1961. Umangi ulipofutwa mwaka 1962, alishika nyadhifa mbalimbali katika Halmashauri ya Wachagga na wadhifa wake wa mwisho ulikuwa kama Mwenyekiti wa Tume ya Serikali za Mitaa. Alifariki mwezi Mei, 1982.

First published in 1947, this is a comprehensive explanation of the customs and traditions of the Chagga people as told by the Paramount chief of the Chagga people of Kilimanjaro, Tanzania.

International availability:
This book is internationally distributed by African Books Collective

Dimensions 230 × 147 mm
Binding

Pages

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Maisha ya Mchagga Hapa Duniani na Ahera”

Your email address will not be published. Required fields are marked *