Mkuki Na Nyota Publishers

Kirusi Kipya

Sh 20,000

Halfani Sudy

Wakina Daniel waliitikia kwa kutikisa kichwa. Rais Mark aliwaangalia Joash Mtoto na Aneth waliokaa katika sofa moja, alitabasamu, kisha akasema huku akim geukia Daniel, “Daniel umefika wakati sahihi wa wewe nawe kuoa. Nipo tayari kuwa baba yako katika ndoa yako. Chagua tu, unamuoa nani kati ya Hannan Halfani au Inspekta Jasmin,” “Kichwa, maneno ya Mheshimiwa Rais ni agizo maalum la Serikali.” Inspekta Jasmin alisema huku akicheka akiwa kwa pembeni. “Cheupe, umepata pa kunishikia sasa,” Daniel alisema huku naye akicheka. Hannan alimwangalia Daniel Mwaseba huku akitabasamu. “Rais akiwa baba yako katika ndoa yako, ina maana Daniel utakuwa “Mtoto wa Rais,” Martin alisema huku akita basamu. “Mtoto wa Rais!” Inspekta Adrian na Binunu walisema kwa pamoja huku wakimwangalia Daniel. Wote wakacheka. Kujua nini kilichotokea zama ndani katika mistari ya kurasa za Riwaya hii.

Kuhusu Mwandishi

Halfani Sudy, ni mwandishi wa riwaya aliyezaliwa mnamo mwaka 1989, mkoani Lindi katika wilaya ya Kilwa. Tangu mwaka 2014 alipomaliza elimu yake ya chuo kikuu, hadi leo, Halfani amefanikiwa kuchapisha vitabu vitano. Miongoni mwa riwaya maarufu za Halfani Sudy zilizochapishwa ni Penzi Chungu, Farida, Kipepeo Mwekundu, Kanda ya Siri na Msako Hatari. Mswada 2022, aliibuka mshindi wa kwanza katika Tuzo ya Safal Cornell ya Fasihi ya Afrika katika kipengele cha riwaya. Kwa sasa, Halfani Sudy ni mkuu wa idara ya ustawi wa jamii na mwalimu wa ustawi wa jamii katika chuo cha  MGM Health and Training Institute kilichopo Iringa mjini (Kitwiru).

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Kirusi Kipya”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…