Haikuwa kazi yake kujishughulisha na makosa ya jinai. Hivyo alishangaa kidogo Chifu alipomwamuru afuatilie tatizo la upungufu wa almasi. Isingekuwa kwa sura aliyoonyesha, angeweza hata kumjibu kuwa apeleke malalamiko yake kwa Kamishna wa Polisi au ampe uhamisho kwenda huko kama alikuwa hamhitaji katika idara yake.
Siku hiyo, Chifu alivaa sura ya kutisha na Willy Gamba hakuwa na la kufanya ila kukubali. Kulikuwa na ushahidi kwamba almasi zilizouzwa katika masoko ya nje zilikuwa chache sana kulinganisha na kiasi kilichokuwa kinachimbwa. Kwa nini iko hivyo!? hilo ndilo suala lililomsumbua sana Chifu.
Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai imejitahidi bila mafanikio. Askari Polisi, Joel, amegusa chanzo cha uhalifu, akafa na uhalifu ukaendelea.
Chifu anamtuma mpelelezi Jack Mbwile, naye maiti yake inaokotwa ikielea katika Ziwa Victoria. Sasa jambo limekuwa zito na hakuna jinsi, lazima Willy Gamba ahusike…
Reviews
There are no reviews yet.