Diwani hii ina mashairi mesto yatakayomwezesha msomaji kujitanua bila ukinzani wa uguni na usiguni, usasa na umapokeo; hivyo azingatie fani, maudhui na muktadha. Dhana zilizodokezwa ni ukoloni mamboleo, usaliti, mila potofu, ukatili, unyanyasaji wa kijinsia, haki za mtoto, UKIMWI, rushwa, kiwi ya akili, uwajibikaji na nyinginezo.
Christopher Bundala Budebah alizaliwa mwaka 1956 huko Maswa, Simiyu. Ni muhitimu wa M.A Kiswahili, Stashahada ya Uzamili ua Ualimu, Shahada ya Kwanza ya Sanaa za Maonyesho na Cheti cha Sanaa za Maonyesho.
Mbali na tuzo ya Mabati, mwandishi aliwahi pia kushinda tuzo ya uandishi wa kazi za fasihi kwenye shindano la Jubilei ya miaka 75 ya TUKI.
Kuhusu Mwandishi
Christopher alizaliwa mwaka 1956 huko Maswa, Simiyu Tanzania ni mhitimu wa M.A Kiswahili, Stashahada ya Uzamili ya Ualimu, Shahada ya Kwanza ya Sanaa za Maonyesho na Cheti cha Sanaa za Maonyesho. Ameshiriki makongamano ya Kiswahili ya Kimataifa huko Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala Uganda. Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya na Chuo Kikuu cha Mtakatifu John, Dodoma Tanzania. Ametoa makala katika jarida la Kiswahili la Kioo cha Lugha “Mbinu za Utunzi wa Nyimbo Ndefu za Wigashe”.
Reviews
There are no reviews yet.