Mkuki Na Nyota Publishers

Hofu

Author(s): A.E. Musiba, apartheid, fasihi ya Kiswahili, riwaya ya Kiswahili, Southern Africa liberation, Swahili novel, thriller, Willy Gamba

Sh 8,000

Mpelelezi Willy Gamba, mhusika maarufu wa mwandishi wa Kiswahili A. E. Musiba, anapambana na makaburu wa Afrika Kusini wanaopanga kuharibu mkutano wa wapigania uhuru unaofanyika mjini Arusha, Tanzania. Mauaji ya kikatili Uitenhage, makaburu walio na hofu ya kupinduliwa, na magaidi wasaliti wa UNITA. Riwaya ya kusisimua: mwindaji awa mwindwaji.

Riwaya ya Kiswahili ya A. E. Musiba inayotumia mhusika maarufu wa mwandishi, mpelelezi Willy Gamba. Mauaji ya kikatili yanafanyika karibu na mji wa Uitenhage nchini Afrika Kusini, siku ya kuwakumbuka wazalendo waliouawa Sharpeville mwaka 1960. Makaburu wanatishiwa na kujawa na hofu, wakitilia shaka njama za kikundi cha watu weusi kutaka kupindua serikali yao ya kibaguzi. Viongozi wa jeshi la usalama na magaidi wasaliti wa UNITA wanapanga wimbi la mauaji kuharibu mkutano wa wapigania uhuru wa Afrika Kusini unaofanyika Arusha, Tanzania. Umoja wa wapigania uhuru unaandaa kikundi makini. Mpelelezi nguli wa Afrika, Willy Gamba, na wenzake kutoka nchi za kusini mwa Afrika wanakabiliana na makaburu na vikundi vya kigaidi. Hekaheka zinatokea Arusha. Mwindaji awa mwindwaji.

Weight 0.3 kg
Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Pages

Year published

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Hofu”

Your email address will not be published. Required fields are marked *