Diwani ya ushairi ya Kiswahili iliyoandikwa kwa lahaja ya Kimvita (lahaja izungumzwayo jijini Mombasa) na Ahmed Hussein Ahmed, mshindi wa Tuzo ya Safal-Cornell ya Fasihi ya Afrika. Lahaja ya Kimvita imetumiwa na washairi maarufu na wazoefu wa tungo katika nyakati mbalimbali kihistoria, kama vile Shaha Muyaka wa Muhaji, Ahmad Nassir Juma Bhalo, Abdilatif Abdalla, na sasa Ahmed Hussein Ahmed. Hii ni lahaja yenye manyumbulifu anuwai kwa namna sauti zake zinavyoleta maana tofauti zinapotamkwa, na ina ukwasi wa misamiati. Mashairi yaliyomo katika diwani hii yanaangazia mada mbalimbali zikiwemo utamaduni wa mwandishi, masuala ya maisha, mijadala ya kielimu, maswali na majibu, taanasi, na masuala ya kisasa. Vilevile mshairi ametumia mbinu mbalimbali za tasnifu ya tungo, kwa mfano tathlitha, tarbia, na majibizano kufikisha ujumbe wake. Diwani inaweka Kimvita katika mfululizo wa kihistoria wa fasihi ya Pwani.

Haile Ngoma ya Wana: Diwani ya Mwanamvita
Author(s): Abdilatif Abdalla, Ahmad Nassir Juma Bhalo, Ahmed Hussein Ahmed, diwani, Kimvita, Mombasa, Muyaka wa Muhaji, Safal-Cornell
Sh 10,000
Diwani ya ushairi ya Kiswahili ya Ahmed Hussein Ahmed, mshindi wa Tuzo ya Safal-Cornell, iliyoandikwa kwa lahaja ya Kimvita ya Mombasa. Inaweka Ahmed katika mfululizo wa Muyaka wa Muhaji, Ahmad Nassir Juma Bhalo, na Abdilatif Abdalla. Tathlitha, tarbia, na majibizano katika tungo zake.
| Dimensions | 195 × 130 mm |
|---|---|
| Binding |
You may also like…
-

The African Epic Controversy
Sh 45,000




Reviews
There are no reviews yet.