Mkuki Na Nyota Publishers

Haile Ngoma ya Wana: Diwani ya Mwanamvita

Authors: Ahmed Hussein Ahmed

Sh 10,000

Ahmed Hussein Ahmed

Diwani hii imeandikwa kwa lahaja ya Kimvita, lahaja izungumzwayo jijini Mombasa. Lahaja hii imetumiwa na washairi maarufu pamoja na wazoefu wa tungo katika nyakati mbalimbali kihistoria kama vile Shaha Muyaka wa Muhaji, Ahmad Nassir Juma Bhalo, Abdalatif Abdalla na sasa Ahmed Hussein Ahmed.
Hii ni lahaja yenye manyumbulifu anuwai kwa namna sauti zake zinavyoleta maana tafauti zinapotamkwa na ina ukwasi wa misamiati. Mashairi yaliyomo kwenye diwani hii yanaangazia mada mbalimbali zikiwemo, utamaduni wa mwandishi, masuala ya maisha, mijadala ya kielimu, maswali na majibu, taanasi na masuala ya kisasa. Vile vile mshairi ametumia mbinu mbalimbali za tasnifu ya tungo kwa mfano, tathlitha, tarbia na majibizano kufikisha ujumbe wake.

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Haile Ngoma ya Wana: Diwani ya Mwanamvita”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…