Mkuki Na Nyota Publishers

Dhulma

Authors: Abdulrazak Gurnah, Dr. Ida Hadjivayanis

Abdulrazak Gurnah (Author)
Translated by Dr. Ida Hadjivayanis

Katika mitaa ya Zanzibar na Dar es Salaam, maisha ya vijana watatu–Badar, Karim, na Fauzia–yanasukwa na matukio yasiyotabirika. Badar, kijana maskini asiye na mizizi wala elimu, anajikuta katika dunia ya watu wenye mamlaka na mali. Akiwa mtumishi, bahati inampiga mawimbi anapokutana na Karim–kijana wa mama mwenye nyumba, mwenye ndoto na matarajio makubwa. Wakati huo huo, Fauzia, bado akiwa kaelemewa na changamoto za utotoni, anatafuta njia ya kujinasua.
Vijana hawa wenye njozi tofauti lakini mustakabali uliofungamana, wanapita kwenye safari ya mapenzi, kazi na uzazi, huku urafiki wao ukijaribiwa na tamaa, hofu, mabadiliko ya kiuchumi na teknolojia na hatimaye–usaliti. Je, hatima yetu huamuliwa na hadhi ya kuzaliwa kwetu, au tunaweza kuiandika upya? Hakika simulizi hii inatupeleka kwenye safari ya maisha ya wale wanaotafuta nafasi yao katika ulimwengu unaobadilika haraka, usio na huruma na wenye dhulma bila kujali walipotoka.
Hii ni Tafsiri ya Riwaya ya Kwanza ya Abdulrazak Gurnah baada ya kutunukiwa Tuzo ya Nobel ya Fasihi ya mwaka 2021.

Dkt. Ida Hadjivayanis ni Mhadhiri Mwandamizi wa Masomo ya Kiswahili SOAS (The School of Oriental and African Studies) Chuo Kikuu cha London. Hii ni tafsiri yake ya pili kwa riwaya za Abdulrazak Gurnah ikitanguliwa na riwaya ya Peponi.

Weight 0.4 kg

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Dhulma”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…