Mkuki Na Nyota Publishers

Historia ya Kiziba na Wafalme Wake

Sh 45,000

Galasius B. Kamanzi and Peter R. Schmidt

Historia ya Kiziba na Wafalme Wake: Tafsiri ya Amakuru Ga Kiziba na Abakama Bamu ni mchango mkubwa kwa fasihi ya kihistoria ya wenyeji wa Afrika ya Mashariki na Tanzania. Utafiti wa Mfalme Mutahangarwa wa Kiziba (aliyetawala 1903–1916) katika mwanzo wa karne ya ishirini ulikusanya mabingwa wasimulizi za mdomo kutoka katika koo za kifalme na zisizo za kifalme na shuhuda zao ziliandikwa na watu waliokwisha kujua kusoma na kuandika, akiwemo F.X. Lwamgira.

Miongo mine baadaye matokeo ya utafiti huo yalipigwachapa kikatokea kitabu chenye kurasa 490 katika lugha ya Kihaya ambacho kilibaki bila kujulikana ingawa kilikuwa kitabu muhimu. Tafsiri hii muhimu itafanya historia ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania na Kusini Magharibi mwa Uganda kabla na mwanzoni mwa ukoloni iwafikie kwa mara ya kwanza wasomi wengi.
Kuhusu Waandishi
Galasius B. Kamanzi ni msomi wa siku nyingi wa historia ya Kiziba na utamaduni wa Kihaya. Ni mwalimu na mtumishi wa serikali mstaafu. Ana shahada ya kwanza ya Ualimu wa Uchumi na Lugha kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam na Stashahada ya Juu ya Uongozi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe. Ni mtunzi-mwenza wa Folktales from Buhaya.

Peter R. Schmidt ni Profesa Mstaafu wa Anthrolopojia katika Chuo Kikuu cha Florida na ni Profesa wa Kuazima wa Anthropolojia Akiolojia katika Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika ya Kusini. Ametunga na/au kuhariri vitabu 15 kuhusu Historia ya Afrika, simulizi za mdomo, urithi na historia ya kuchimba, vingi kati ya hivyo vikihusu Wahaya.

International availability:
This book is internationally distributed by African Books Collective

Dimensions 210 × 130 mm
Binding

Pages

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Historia ya Kiziba na Wafalme Wake”

Your email address will not be published. Required fields are marked *