Mkuki Na Nyota Publishers

Changa la Macho

Author(s): Fatuma Salim

Sh 10,000

ISBN: 978-9987-08-629-0 Categories: , , , , , Tag:

Tunaishi katika jamii inayoshuhudia maovu, dhuluma, ukatili, ufisadi na unyanyasaji kila siku. Tunaona. Tunajua. Lakini tunakaa kimya. Ukimya huo unamlinda nani? Na kwa gharama ya nani? Kupitia diwani hii, Fatuma anatualika kulifuta changa linalofumba macho yetu ili tuyaone yale yanayofichwa na hofu pamoja na mazoea. Anatukumbusha kuwa ukweli haupotei hata kama ukipuuzwa.

Mbali na kuibua changamoto zinazoikabili jamii, mwandishi pia anasherehekea mema yanayopaswa kuhifadhiwa: lugha yetu, mshikamano, upendo na maadili yanayojenga taifa. Hivyo, ushairi unakuwa si sanaa ya maneno pekee, bali sehemu ya turathi ya jamii inayohifadhi historia, utamaduni na maadili yanayorithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Kuhusu Mwandishi

Fatuma Salim ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA). Ni mwandishi wa mashairi, tenzi, hadithi za watoto na hadithi fupi. Amechangia uandishi wa vitabu mbalimbali, vikiwemo Ndimi Zenye Ncha, Malenga wa Afrika, Wosia wa Washairi na Kilinge cha Ukombozi.

Weight 0.1 kg
Dimensions 195 × 130 × 7 mm

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Changa la Macho”

Your email address will not be published. Required fields are marked *