Mkuki Na Nyota Publishers

Nyaraka za Wafu

Author(s): Ali Othman Masoud

Sh 15,000

ISBN: 978-9987-08-622-1 Categories: , , , , Tag:

Mahir, mtaalamu wa masuala ya Nyuklia na akili unde kwenye kampuni za kigeni, anajitosa kufanya utafiti wa nani hasa yupo nyuma ya uwepo wa kirusi cha FUR+ ambacho kinaua watu wengi nchini akiwemo Asumin, mwanamke aliyempenda kwa dhati tangu wakiwa wadogo.

Mahir anajivisha ujasiri ambao, hata ikibidi uhai wake uondoke. Anapambana kuubaini ukweli wa nani yupo nyuma ya kirusi hicho hatari. Pengine hakuwa ametambua nguvu halisi ya wahusika hao alipojitosa ndani ya uchunguzi wake, mpaka pale mambo mazito yalipoanza kumtokea yeye na watu wake wa karibu. Je, ataendelea na msimamo wake? Je, atafanikiwa kutimiza azma yake? Sasa endelea.

KUHUSU MWANDISHI

Ali Othman Masoud ni mtafiti mwandamizi wa fizikia ya mionzi na nyukila. Pia ni mwandishi wa fasihi na mchambuzi wa mambo ya jamii kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kutoka Zanzibar. Anahudumu katika Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), akijishughulisha na usalama wa mionzi, utafiti, na uboreshaji wa huduma za afya kupitia teknolojia ya kisasa ya akili unde. Mbali na taaluma ya sayansi, anafahamika pia kwa jina la kalamu Ben Othman, akiwa mwandishi mahiri wa riwaya, mashairi, na makala zinazolenga kuhifadhi, kuendeleza na kuenzi lugha na utamaduni wa Kiswahili.

Weight 0.4 kg
Dimensions 195 × 130 × 16 mm

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Nyaraka za Wafu”

Your email address will not be published. Required fields are marked *