Mkuki Na Nyota Publishers

Bweni la Wasichana

Author(s): Buibui, Kibaha, Kiswahili, Lucas Lubago, riwaya, Safal-Cornell, Safal-Cornell 2021, shule

Sh 15,000

Riwaya ya kwanza ya Lucas Gervas Lubago, iliyoshika nafasi ya pili katika Tuzo ya Safal-Cornell ya mwaka 2021. Hadithi ya mwalimu anayegundua aibu kubwa bweni la wasichana. Mwandishi ni mwalimu wa biashara aliyesoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Riwaya ya kwanza ya Lucas Gervas Lubago, iliyoshika nafasi ya pili katika Tuzo ya Safal-Cornell ya mwaka 2021. Usiku huo nilikuwa nasimamia maandalizi ya masomo ya usiku. Nikapigiwa simu na Rose, nikaipokea. Wakati naongea naye, nikawa natembea taratibu kama naelekea kwenye mabweni. Ghafla, nikaona taa za bweni wanalolala Buibui zinawaka na kuzima; nikajua ni hitilafu katika mfumo wa umeme. Nikataka kusogea ili nithibitishe, kisha nitoe taarifa mapema kwa uongozi na matengenezo yafanyike. Nilisogea mpaka mlangoni, taa zikawaka moja kwa moja, na kwa kuwa kulikuwa na dalili za kuwemo mwanafunzi, nilitaka kujua kwa nini hayupo darasani. Niliingia nikakuta hali ya ukimya sana, nikatembea mpaka karibu na mwisho wa bweni, nilichokiona ni aibu kubwa. Lucas Lubago ni mwalimu wa masomo ya biashara (Accountancy and Commerce). Alisoma Sekondari ya Wavulana ya Kibaha na alipata elimu ya juu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Dimensions 195 × 130 mm
Binding

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Bweni la Wasichana”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like…