Tafsiri ya Kiswahili ya utendi The Perfect Nine, ulioandikwa na mwandishi mashuhuri Ngugi wa Thiong’o, iliyofanywa na Ndirangu Wachanga. Utendi unahusu chimbuko la jamii ya Agikuyu (Wakikuyu). Kitovu cha jamii hii ni wazazi watangulizi Gikuyu na Mumbi, na mabinti zao tisa. Maisha ya familia hii anzilishi yanachambua maudhui mengi kwa kina yakiwemo ustahimilivu wa changamoto za kusaka maana ya maisha, maadili, uvumilivu, na nguvu ya upendo wa kweli katika kufanikisha ndoto, ujasiri, matumaini, na ushindi. Kutokana na uzuri wa mabinti hao na sifa zao za kipekee, waliwavutia vijana wengi waliotaka kuwaoa. Vijana 99 wanapewa nafasi, lakini kwa kutimiza masharti magumu yanayopelekea baadhi yao kupoteza maisha. Je, vijana gani watafanikiwa kuwaoa mabinti hao na kwa nini? Tafsiri ya Kiswahili ya kazi ya mmoja wa waandishi mashuhuri zaidi wa Afrika, mwana wa harakati ya fasihi za lugha za Kiafrika.

Tisa Timilifu
Author(s): Agikuyu, Gikuyu na Mumbi, Ndirangu Wachanga, Ngũgĩ wa Thiong'o, tafsiri, The Perfect Nine, utendi, Wakikuyu
Sh 10,000
Tafsiri ya Kiswahili ya utendi The Perfect Nine wa Ngugi wa Thiong’o, iliyofanywa na Ndirangu Wachanga. Chimbuko la jamii ya Agikuyu kupitia Gikuyu, Mumbi, na mabinti zao tisa. Vijana 99 wanapewa masharti magumu kuwaoa. Tafsiri ya kazi ya mmoja wa waandishi mashuhuri zaidi wa Afrika.
| Dimensions | 195 × 130 mm |
|---|
You may also like…
-

Faradhi Ya Moyo
Sh 18,000 -

Voice of Agony
Sh 40,000





Reviews
There are no reviews yet.